filmov
tv
WITO WA KUTAZAMA JUU

Показать описание
Moja kati ya ukweli wa wakati huu, ni kile kinachoendelea katika huduma ya Yesu Patakatifu pa Patakatifu. Katika somo hili utagundua kuwa, hatua mbili za huduma ya Yesu, yaani Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu zitachukua jumla ya miaka elfu mbili (2000), na ndiyo miaka elfu mbili (2000) ya uwepo wa kanisa la Kristo duniani kabla ya mwisho wa dunia. Katika somo hili, tunajulishwa ya kwamba muda umeisha na Yesu amekaribia sana kurudi. Huu ni ujumbe wa siku hizi za mwisho kwa Waadventista wa Sabato ya kwamba, imebaki miaka saba (7) tu. Yale matukio makubwa ya Kinabii yanayoshikamana na kufungwa kwa mlango wa rehema yatatimia mbele ya macho yetu, hakika kizazi hiki hakitapita. Somo hili ni muitikio wa wito wa Bwana, ya kwamba, sasa ndio wakati wa kuwaambia watu wapi tumefka katika historia ya kinabii na walinzi tunapaswa kupaza sauti kwa mlio maalumu. Nabii anasema hivi; "Wakati ulimwengu wa Kiprotestanti kwa mtazamo wake unafanya makubaliano na Rumi, hebu tuamke na kuelewa hali na kuona mashindano yaliyo mbele yetu katika uhalisia wake. Hebu walinzi sasa wapaze sauti zao na kutoa ujumbe ambao ni ukweli wa wakati huu. Hebu tuwaonyeshe watu wapi tumefika katika historia ya kinabii na tutafute kuamsha roho ya Uprotestanti wa kweli……...” {5T 716.2}. Kwa kweli Uprotestanti umeshafanya makubaliano na Rumi, na jumapili itapitishwa hivi karibuni. Bwana akubariki unapoendelea kufuatilia masomo haya, usisahau ku-subscribe na ku-share.
Комментарии