Hali Ilivyokuwa Leaders Club Baada Ya Fiesta Kuhairishwa

preview_player
Показать описание
Kamati ya maandalizi ya tamasha la Fiesta imesema tamasha hilo halitafanyika leo Jumamosi Novemba 24, 2018 kama ilivyopangwa, kwamba wananchi waliolipa viingilio watarejeshewa fedha zao.

Kamati hiyo imeeleza hayo leo ikiwa ni saa chache baada ya manispaa ya Kinondoni kuzuia tamasha hilo kufanyika katika viwanja vya Leaders Club.

Kupitia barua inayosambaa katika mitandao ya kijamii manispaa hiyo imesema kuwa tamasha hilo limehamishiwa katika viwanja vya Tanganyika Peakers, badala ya Leaders Club.

Sebastian Maganga, mwenyekiti wa kamati ya Fiesta ametoa tamko la kusitishwa kwa tamasha hilo leo, akieleza kuwa waliolipa kiingilio watarejeshewa fedha zao.

“Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kusitisha tukio la kilele cha msimu wa Tigo Fiesta 2018 lililopaswa kufanyika leo Novemba 24, 2018 katika viwanja vya Leaders Kinondoni Dar es Salaam. Sababu za kusitishwa kwa tamasha hili zipo nje ya uwezo wetu,” anaeleza Maganga.
Рекомендации по теме
Комментарии
Автор

Ikiwa mlango mmoja umefungwa juwa kuwa kuna mengine kumi ipo wazi karibu kitakuja kitu kikubwa kutoka cloud fm

abdulsamadabdulkheir