MAMBO 10 KESI YA MBOWE, MAPYA YAIBUKA, MAJAJI WAJA KIVINGINE, OMBI LA PINGAMIZI LATUPILIWA MBALI..

preview_player
Показать описание
MAMBO 10 KESI YA MBOWE, MAPYA YAIBUKA, MAJAJI WAJA KIVINGINE, OMBI LA PINGAMIZI LATUPILIWA MBALI..

Mahakama Kuuu Divisheni ya makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imepanga kusikiliza kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya Msingi ya Uhujumu yenye mashtaka ya kula njama na kutenda vitendo vya kigaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu.
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Utetezi Fredrick Kiwelo pamoja na Mawakili wenzake, kupinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo, Mohamed Ling'enywa.

Maelezo hayo ya onyo yalitolewa Leo na shahidi wa nane katika kesi hiyo, Mrakibu wa Polisi Jumanne Malangahe, ambaye aliomba mahama hiyo ipokee maelezo hayo ili yatumike kama kielelezo katika kesi hiyo.

Katika ushahidi wake SP Malangahe alidai kuwa alichukua maelezo ya Ling'wenya , Agosti 7, 2020 katika kituo Kikuu Cha Polisi Dar es Salam.
Hata hivyo, Upande wa utetezi walipinga kielelezo hicho kisipikelewe na Mahakama kwa kuwasilisha hoja mbalimbali zikiwemo za Ling'enywa haluchukiliwa maelezo yake Kituo hicho Kikuu Cha Polisi Dar es Salama, pia alitishiwa na Silaha wakati akiwa kituo cha Polisi Mbweni wakati alilazimishwa kusaini maelezo ambayo hakuyaandika.

Pia mawakili hao wamedai kuwa maelezo ya mtuhumiwa huyo yalichukuliwa nje ya muda unaoruhusiwa kisheria ambao ni masaa manne tangu kukamatwa kwa mtuhumiwa.

Wakili Serikali Robert Kidando amedai wamepitia mapingamizi hayo nakudai kuwa mapingamizi mawili kati ya tano yaliyotolewa na Mawakili wa utetezi ndiyo yenye mashiko hivyo kuomba muda wa kuajiandaa na kesi ndogo ndani ya kesi kubwa.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:

⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 712 101 629), ( +255 784 888982)

⚫️ OUR PLAYLISTS:
Рекомендации по теме
Комментарии
Автор

Nyie endeleeni kubishana na mtoa haki kwa kujifanya kama hamjui haki iko wapi mungu yupo atatenda miujiza yake

kennyrogers
Автор

Macomando mnashindwa kufanya maajabu mko 3 mmetekwa na raia

sagilododomamedelipeter
Автор

Majaj au jaj kwan wanaosikiliza kesi ni wangapi sini mmja au?

ellymichael
Автор

Yani hii kesi kama anavyo dai Le bac mawakili wangejitoa tu Ili huyo jaji amfuñge kama wanavyo taka

mohamedkigwehe
Автор

Mboe Ni gaidi mkubwa katika inchi yetu Bora lifungwe tu hilo jambazi

shaabanshaaban