MAPINGAMIZI KESI YA MBOWE YATUPWA TENA, KESI INAENDELEA...

preview_player
Показать описание
MAPINGAMIZI KESI YA MBOWE YATUPWA TENA, KESI INAENDELEA

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali hoja tatu zilizotolewa na upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi na kukipokea kitabu cha kumbukumbu ya mahabusu kama kielelezo.

Uamuzi huo ulihusu pingamizi la mawakili wa utetezi katika kesi hiyo, ambao walipinga kupokewa kwa kitabu cha kumbukumbu za mahakama (Detantion Register – DR), cha Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam, cha mwaka 2020, kiwe kielelezo cha ushahidi upande wa mashtaka.

Ikimbukwe kuwa upande wa mashtaka unaongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando uliiomba mahakama hiyo ikipokee kitabu hicho kuwa kielelezo cha ushahidi wake, kupitia kwa shahidi wa pili katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, Ditektivu Koplo Ricardo Msemwa.

Kwa upande wao upande wa utetezi unaongozwa na Peter Kibatala ambao ulikuwa ukipinga kitabu hicho kupokewa, huku wakitoa hoja tatu za pingamizi lao ambapo walikuwa wakidai kwamba hakuna amri ya mahakama ya kukiondoa mahakamani kielelezo hicho kwa kuwa kilishapokewa mahakamani katika kesi ndogo iliyohusu uhalali wa maelezo ya mshtakiwa wa pili, Adamu Kasekwa.

Wakatia jaji Joachim Tiganga akitoa uamuzi wake huo mdogo amesema kuwa

Mahakama inaweza kutoa amri ya kutoa kielelezo pale ambapo shauri limefika mwisho au rufaa imefika mwisho.



Jaji Tiganga akaendelea kusoma hoja mbalimbali za pande zote mbili ambazo zilitolewa na mwisho jaji akasema kuwa kwa maana hiyo anatupilia mbali sababu zote tatu za mapingamizi ya kuzuia kielelezo hicho kutokupokelewa na kesi ikaendelea na usikilizwaji na ushahidi.

Mbowe na wenzake hao, Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa na Mohamed Abdillahi Ling’wenya wanakabiliwa na kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Joachim Tiganga ambapo hadi sasa inaendelea na Ushahidi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:

⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 712 101 629), ( +255 784 888982)

⚫️ OUR PLAYLISTS:
Рекомендации по теме
Комментарии
Автор

Jamen iv nyie majaj iv mko je?jamen mbona ivi au mnafurahia binadam kuteswa gelezan jamen tenden haki

ellymichael