filmov
tv
Ziara ya Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi katika ofisi za LATRA CCC.
Показать описание
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David M. Kihenzile(Mb.), alifanya ziara katika ofisi ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini jana, tarehe 25-01-2024, ambapo alipata fursa ya kujifunza kwa kina jinsi Baraza linavyotekeleza majukumu yake. Aidha, alisisitiza umuhimu wa Baraza kuendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa watumiaji wa huduma za usafiri ardhini katika mikoa yote ya Tanzania, kutayarisha ripoti za utendaji kazi, kuimarisha juhudi za kujitangaza, na kufanya tafiti mbalimbali kuhusu huduma za usafiri wa ardhini.