Aliempiga kibao Ali Hassan Mwinyi afariki dunia.

preview_player
Показать описание
SHUJAA IBRA!

Jumanne ya March 10 mwaka 2009 kijana Ibrahim Saidi (pichani) maarufu kama "Sultani" alimzaba kibao Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, wakati wa baraza la Maulid katika ukumbi wa Diamond Jubilee, tukio lililoibua taharuki kubwa ukumbini hapo na nchi nzima kwa ujumla.

Baada ya tukio hilo Mzee Mwinyi alisema amemsamehe kijana huyo, lakini Polisi walimkamata na kumfungulia mashtaka ya shambulio la kudhuru mwili. March 11 alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, ambapo alikiri kosa na kufanya shauri hilo kusikilizwa kwa siku moja tu kabla ya kutolewa hukumu.

Ibra alisema sababu ya kumtandika kibao Mzee Mwinyi ni kutokana na kuzungumzia masuala ya kondomu kwenye baraza la Maulidi ambapo ni kinyume na mafundisho ya dini yake. March 13 mwaka 2009 Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Neema Chusi, alimhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela.

Kabla ya kusomewa hukumu hiyo Ibra alipewa nafasi ya kuiomba mahakama impunguzie adhabu lakini alisema mahakama hiyo haina uwezo wa kumpunguzia adhabu isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee.
_
“Mimi ni kiumbe dhaifu, hakimu ni kiumbe dhaifu, na sote ni viumbe dhaifu mbele ya Mwenyezi Mungu. Siwezi kuiomba mahakama inipunguzie adhabu, ila namuomba Mwenyezi Mungu anipunguzie adhabu ya kaburi. Na kama akitaka nipunguziwe adhabu mnayotaka kunipa hakuna wa kuzuia” alisema Ibra.

Baada ya kutumikia adhabu yake kwa miezi 8 alipata msamaha wa Rais na kuachiwa huru, lakini June 02 mwaka 2019 alifariki dunia nyumbani kwake Mabibo Loyola jijini Dar.!
Рекомендации по теме
Комментарии
Автор

INNA LILLAH WAINA ILAIH RAJIOUN MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI AMEEN YA RABI ALLAMEEN IN SHAA ALLAH

abdulrahmansalim
Автор

Inna lillah wainna ilayhi raajiuun. Kijana aliteleza kama binaadam kumpiga baba yake kibao amefanya kosa kumpiga baba yake. Baba wa mwenzio ni baba Yako. Ahsanteni kwa ushirikiano.

yusuphmohamed
Автор

Allah ampe nuru na ampunguzie adhabu ya kaburi huko endako

KatotoTraders
Автор

ALLAH AMPE KAULI THAABIT NA AMPUNGUZIE ADHABU ZA KABURINI NA AMPE JANNAH AKIPENDA

rajabngai
Автор

Una uhakika ni bangi au ni maneno aliyoyazungumza yalimudhi ndio akachukua hatua hiyo sio bangi kabisa kuhalalisha zinaa dhana ni mabaya unasema kitu huna uhakika nacho

EshaHamd-edyv
Автор

Mungu ampe pepo shujaa huyo... Alikemea uovu kwa mkono wake

yusufmohamed
Автор

Lakini hii dunia kuna minjemba ya ajabu sana

Dymitri-Babushka.
Автор

Aaagh, kuna watu hata kujilipua hawashindwi aisee

vintagemusicgroup
Автор

Hivi walinzi.wake walikuwa wapi ni wa kufukuza kazi

asteriashios
Автор

Sasa hawa mabodigadi Ndio vipi, inafikia mpaka kiongozi anapigwa wao hawaelewi, je angelikua ana kisu au spoki je??? Ulinzi mwepesi mno

saidrakwe
Автор

Eeeh mola wetu yaonee mapenz yetu juu ya mja wako tunakuomba umuondolee adhabu ya kaburin na umpe daraja ulipendalo uko mbinguni

RizzyKiboko