filmov
tv
SAKATA LA P DIDDY PICHA ZAKE ZAVUJA ALIKUWA AKILA CHAKULA KILICHOTENGWA KWENYE MWILI WA ...
Показать описание
Msanii wa Hip Hop nchini Marekani, Sean ‘Diddy’ Combs maarufu kama P Diddy ameendelea kuteka mitandao ya kijamii na hii ni baada ya picha nyingine kuvuja zikimuonyesha akila chakula kilichotengwa kwenye mwili wa mwanamke ambaye yuko ‘Utupu’ yaani yuko uchi.
Diddy alikamatwa nchini humo akikabiliwa na mashtaka kadhaa yakiwemo ya usafirishaji haramu wa binadamu na utumikishaji wa wanawake kwenda kuwafanyisha vitendo vya ngono.
Tangu kukamatwa kwake P Diddy amekuwa akishika vichwa vya habari kutokana na watu wengi waliowahi kushiriki katika sherehe zilizokuwa zinaitishwa katika majumba yake yaliyopo nchini humo wakidai kuwa msanii huyo amekuwa akitenda vitendo ambavyo ni vya aibu hata kuvitaja mbele ya Umma ikiwemo unyanyasaji wa kingono.
Miongoni mwa sherehe ama ‘Party’ ambazo zilizoratibiwa na msanii huyo ambayo sasa inatembea kwa kasi mitandani ni leo Ijumaa Septemba 27,2024 ni ile ambayo anaonekana akiwa ametengewa chakula kwenye kifua cha mwanamke ambaye yuko utupu.
Katika picha hiyo, Diddy mwenye umri wa miaka 54, anaoneka akiwa amevaa nguo nyeupe akiwa amesimama pembeni ya mwanamke huyo ambaye hata hivyo sehemu zake za siri zilikuwa zimefichwa kwa kutumia jani kubwa la mmea.
Wakati hayo yakiendelea kwenye picha P Diddy anaoneka akichukua na kula zabibu kwenye kifua cha mwanamke huyo ambaye hata hivyo bado hajatambulika jina lake huku mwili wake ukiwa umenakshiwa na matunda mbalimbali zikiwemo zabibu nyekundu.
Katika sherehe hiyo pia kulikuwa na mastaa kama Owen Wilson, Bruce Willis, Will Smith, na Diana Ross hata hivyo bado haijawekwa wazi wapo nao walishiriki kufanya alichokuwa akikifanya P Diddy.
Shauri linalomkabili lilipoitwa mahakamani P Diddy alinyimwa dhamana na badala yake Mahakama apelekwe kizuizini katika gereza la Metropolitan Detention Center in Brooklyn, New York nchini humo, gereza hilo linadaiwa kuwa gereza hatari zaidi kwa usalama wa wafungwa nchini Marekani.
Katika kesi hiyo Diddy, waendesha mashtaka wameieleza Mahakama hiyo kuwa msanii huyo alikuwa akitumia nguvu na ushawishi wake wa kifedha kuwalazimisha wanawake kufanya mapenzi na wanaume na wafanyakazi waliokuwa wakihudhuria katika ‘Party’ mbalimbali alipokuwa akiziitisha katika makasri yake.
Kesi hiyo ilienda mbali na kuwatuhumu waganyakazi wa P Diddy kuwa walihusika katika kurahisisha tafrija hizo kufanyika ikiwemo kununua vilainishi, mafuta y watoto na vipodozi zaidi ya chupa 1,000 zilizokamatwa ndani ya nyumba za Diddy zilizopo jijini Los Angeles na Miami nchini humo.
Kipande cha video kinachohisiwa kurekodiwa takribani miaka 25 iliyopita kimesambaa kikimuonyesha msanii huyo ambaye ni mwanzilishi wa Lebo ya Bad Boys na kinatajwa kuwa miongoni mwa sababu za kukamatwa kwa staa huyo wa muziki wa kufoka maarufu mama Hip Hop.
Kwa nyakati tofauti Diddy amesikika akisema hawatokoma kuandaa tafrija za aina hiyo kama ambayo amenukuliwa akisema;
“Katu hatutokoma, tutaendelea kula bata na kuwaleta watu pamoja kutoka pande zote za dunia. Najua wengine watajaribu kuwafanya wawe kimya wasishiriki,na huenda hata wakanikamata lakini ninachoweza kusema ni kwamba hatutoacha kufurahia maisha,”
Diddy alipoulizwa alikuwa anajisikiaje anapokuwa kwenye tafrija zake hizo, alisema; “Kwa kweli ni nzuri japokuwa hazikunifanya kuwa wa tofauti na wengine lakini zinanifanya nijione kama mtu niliyeyapatia maisha,”
IMEANDALIWA NA KAITIRA

Комментарии