filmov
tv
Je Maumivu ya Tumbo ya kubana na kuachia kwa Mjamzito husababishwa na Nini? | Je ni hatari au lah?
Показать описание
Je maumivu ya Tumbo ya Kubana na Kuachia kwa Mjamzito huwa ni hatari au lah?
Ukweli ni kwamba 90% ya Wajawazito hupata aina hii ya Maumivu ktk kipindi chao cha Ujauzito, inawezekana Miezi Mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito, Miezi Mitatu ya katikati ya Ujauzito au Mwishoni mwa Ujauzito ambapo hupelekea Uchungu kwa ajili ya kujifungua.
Asilimia kubwa ya Wajawazito wanapopata Maumivu haya yasiyo makali sana huwa ni kawaida kutokana na sababu zifuatazo;-
1. Mabadiliko ya Homoni ya kawaida katika kipindi cha mwanzoni mwa Ujauzito, Kutokana na maongezeko ya homoni mbalimbali mfano; Homoni ya Progesterone mwanzoni kabisa mwa Ujauzito.
2. Ukuaji wa Mtoto kwenye Mji wa Uzazi, Endapo Mfuko wa Uzazi unaongezeka hususani kwenye Miezi Mitatu ya katikati ya Ujauzito huweza kupelekea kuvutika kwa Baadhi ya tishu zinazoshikiza Mfuko wa Uzazi na kupelekea maumivu ya Tumbo kwa Mjamzito.
3. Maumivu ya kubana na kuachia kitalaam huitwa Braxton Hicks Contractions ambayo hutokea katika kipindi cha Ujauzito,kwa kawaida maumivu haya huwa hayana Mpangilio maalumu.
4. Uchungu kabla ya Wakati.
Endapo maumivu ya kubana na kuachia yanaongezeka kadiri muda unavyoenda na hutokea Mara kwa Mara huweza kupelekea wakati mwingine kupata Uchungu kabla ya wakati na kujifungua Mtoto asiyekuwa amekomaa vizuri.
5. Maumivu ya kubana na kuachia yanaweza kupelekea Uchungu wa kawaida kwa Mjamzito ambaye Mimba yake imekomaa vizuri au imefikisha miezi 9.
UKIWA NA MAUMIVU YA KUBANA NA KUACHIA AMBAYO YANAAMBATANA NA DALILI ZIFUATAZO UNATAKIWA KWENDA HOSPITALI HARAKA:
Dalili hizo ni Kama;
1. Kutokwa na Damu Ukeni kipindi chochote Cha Ujauzito.
2. Kutokwa na Maji Ukeni katika kipindi chochote kile cha Ujauzito.
3. Maumivu ya Kubana na Kuachia ambayo ni makali zaidi yasiyovumilika kabisa.
4. Maumivu makali ya Tumbo wakati mwingine huashiria kuwa Mimba iko nje ya Mji wa Uzazi na huweza kupasuka katika Mirija ya Uzazi hivyo unahitaji Matibabu na Upasuaji wa dharula.
5. Maumivu ya sehemu ya chini ya Tumbo ambayo huambatana wakati wa kupata haja ndogo yaani kukojoa.
6. Maumivu kwenye Tumbo Sehemu ya juu upande wa kulia kwa wale wenye presha kubwa katika kipindi cha Ujauzito na nk.
Nifuatilie kwenye channel yangu kuhusu Mambo ya Ujauzito.
Nifuatilie Instagram kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito.
Nifuatilie kwenye website hii kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito.
Nifuatilie kwenye Facebook page kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito.
Usisahau kudownload app ya Mama Afya Bora kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito.
©Dr.Mwanyika
#drmwanyika
#mamaafya
#MaumivuKubanaKuachia

Комментарии