MAMA MARIA NI MAMA YETU- Kwaya ya Mt Mikaeli Malaika Mkuu Chang'ombe DSM(Mtunzi Aloyce Kipangula)

preview_player
Показать описание
MAMA MARIA NI MAMA YETU. By Aloyce Kipangula. KWAYA Mt MIKAELI PAROKIA YA CHANG'OMBE JIMBO KUU KATOLIKI DAR ES SALAAM

Mama Maria ni Mama yetu, Mama maria ni mama yetu kwa sababu ameunganika na Yesu mwanaye katika kutukomboa x 2

1 Mama huyu Bikira Maria, yeye ndiye Eva mpya mnyenyekevu na mwenye huruma, mama wa Neema,
Kupitia kwa mama Maria, tulimpata Mkombozi aliyekuja kutukomboa utumwani mwa shetani hivyo mama Maria........

2 Yesu alipomwona mama yake, na mwanafunzi wake Yohane alimwambia Mama tazama, Huyo ndiye mwanao,
Kisha akamwambia Yohane, mtazame mama yako Yohane akamchukua Maria akae nyumbani kwake hivyo Mama....

3 Na katika Harusi ya kana walitindikiwa divai Maria akamwambia mwanaye, hawana divai,
Yesu akamtii mama yake, akawarejeshea furaha kwa kuwa aliyageuza maji yakawa divai hivyo...

4 Hata katika nyakati zetu, tunapungukiwa tunatindikiwa tunamuhitaji yesu katika maisha,
Tumwendee mama Maria, atatuombea kwa Yesu na Yesu atamtii mama yake atatujalia hivyo..
Рекомендации по теме
Комментарии
Автор

Aloyce unapotea sana kwakweli daaah! Umenikumbusha sana nilifundisha misa moja ya Fatima sehemu hadi nimeona raha

simonmisri
Автор

Hongereni sana. Wimbo mzuri mnoo. Hakika mama Maria ni mama yetu

PendoKivyiro
Автор

Tunamshukuru mungu kwa kutuwezesha katika kufanya hili🙏🙏

pendosteven
Автор

Hongereni sana, wimbo mzuri sana, mbarikiwe kwaya ya Mt. Mikaeli chang'ombe mko vizuri mungu azidi kuwabariki mzidi kuinjilisha kwa kupitia nyimbo.amina

ZawadiWilson-bgny
Автор

Mama maria ni mama wa ulimwengu mzima🎉🎉

GraceWanjiru-ie
Автор

Wimbo safi🎉, Wacha tu. Mbarikiwe Sana

nelsonwekulo
Автор

Kazi nzuri Mungu atukuzwe wimbo mzuri sauti Safi mavazi super yaani mbarikiwe daima.

methodbayona
Автор

Hakika ninafarijika Sana na nyimbo zenu hongereni sana mzidi kutuinjirisha kwaya ya mt Michael nilikuwa sijui Ila kwa nyimbo za mama Maria nimewafahamu vyema

ClaraKabendera
Автор

Nyimbo nzuri sana, sare nzuri, Ujumbe mzuri,
Safi sana, mbarikiwe

PaulMbawala-be
Автор

Wimbo mzuri sana. Hongereni sana. Naipenda sana parokia yq Chang'ombe kwa sababu ya uimbaji bora

AndrewCheyo
Автор

Mbarikiwe sana, nyimbo nzuri mno Kwa keeling mama Maria ni mama yetu. Kazi nzuri na mzidi kutuburudisha.katoliki daima❤❤

suekidskidsue
Автор

Hongerani sana ndugu wanakwaya wenzetu Hakika Mmeipiga kwa wingi!

sasinematinda
Автор

Kweli Mama Maria ni mama yetu, hongera kwa uinjilishaji kwa njia ya kuimba

demetriarwiza
Автор

Ulikuwa unaniburudisha na wauzaji flash ni wachangamfu mnoo na wakarimu hongereni❤❤

ChristinaSimao-hxix
Автор

Ngoja niulze mbona hii kwaya wanakwaya wanafanana na ile kwaya ya maria goret chuo kikuu moshi au nimeona vibaya😢

olicej
Автор

Wimbo mtamu sana, hongereni sana kwa utume

peterjohn
Автор

Thanks for the song, blessed I am now.

godfreymaina
Автор

This song uplift my day to day 🙏mama maria zidi kutuombea

chepngetichfreda
Автор

Truelly is our mother She intercedes for us

MUHINDOHANNINGTON-de
Автор

Jaman napenda sana huu wimbo mbarikiwe

AnnaKangombe-zz