Hoja ya utekaji yaibuka tena bungeni, Spika Tulia, Waziri Mkuu wabanwa kutoa maelezo

preview_player
Показать описание
Hoja ya utekaji, mauaji na kupotea kwa watu ikiwemo watoto imeibuka tena bungeni baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonest kutaka mkakati wa Serikali kukomesha matukio hayo aliyodai baadhi yanahusishwa na vyombo vya dola.

Leo Alhamisi, Agosti 29, 2024, hoja hiyo imeibuka bungeni wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, baada ya Anatropia kusema matukio ya utekaji, mauaji na kupotea kwa watu yanaashiria uvunjifu wa haki za binadamu.

Amesema matukio hayo yamekuwa na sura tofauti tofauti ikiwemo wivu wa mapenzi na ushirikina.

“Lakini na matukio mengine ya kutekwa na kupotea kwa watu yanahusishwa na vyombo vya dola. Nataka kufahamu mkakati wa Serikali kuzuia matendo haya lakini kuondoa taharuki ambayo inajitokeza katika jamii,” amesema.

Hata hivyo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kabla ya kumpa nafasi Majaliwa kulijibu swali hilo, amesema juzi Jumanne Agosti 27, 2024 alisimama Mbunge wa Nkasi Kaskazini (Chadema), Aida Khenani akazungumzia suala hilo.

Amesema mambo hayo yanayohitaji uchunguzi:“Leo asubuhi nimesoma kuna mganga amezika watu sijui 10 na ngapi, sasa huyu mganga ni polisi ambaye watu ameuawa na wamezikwa kwake.”

Amesema mambo hayo yakiwa yanasemwa kwa hisia hivyo inakuwa kama mtu hajali wakati kila mtu anajali na kila binadamu ana haki ya kuishi.

“Lakini tusiweke mazingira kwamba kila anayepotea…si kuna mabasi wanapanda kule chini, akidondoka huko chini si nyumbani wanamtafuta utasema ni chombo cha dola kimemchukua.Sisi lazima tuifanye hii kazi kama viongozi ukichukua mihemko hutoi nafasi kwa Serikali kufanya kazi yake wakati huo huo hutoi nafasi kwa jamii kuendelea kushiriki katika jambo,” amesema.

Amesema wao wote ni viongozi na wangependa wananchi wao wawe salama na kuonya mambo hayo yasichukuliwe jumla jumla.

“Na wewe chukua nafasi ya uongozi, unaweza kutoa ushauri lakini usinyooshe vidole kwa sababu huna hakika. Na wengine wanahama nchi si tunakamata hapa kila siku, na wenyewe huko kwao wanatafutwa watasema chombo cha dola kimewachukua kimewapeleka sijui wapi,” amesema.

Amesema huku kwao wanawatafuta wahamiaji hao waliokamatwa nchini lakini kumbe alipofika hapa Tanzania mazingira yamekuwa magumu na hivyo amekamatwa.

Baada ya maelezo hayo ya Spika Tulia, amempa nafasi Waziri Mkuu Majaliwa kueleza akisema jukumu la kulinda nchi ni wajibu wa Watanzania wote kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.

“Tunavyo vyombo vya ulinzi na usalama vyenye jukumu la kupokea taarifa mbalimbali zinazoonyesha uvunjifu wa amani popote pale kwenye meza ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Jukumu lao baada ya kupokea taarifa ni kuhakikisha wanafanya uchunguzi,” amesema.

Majaliwa amesema uchunguzi unapobaini waliotenda makosa, wanawapeleka katika vyombo vya sheria.

Amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kujikita kusimamia misingi ya amani katika nchi yetu na usalama kwa kuhakikisha raia na mali zao zinabaki salama.

Amewahakikishia Watanzania kwamba suala la ulinzi na usalama bado liko mikononi mwao pamoja na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.

“Jukumu letu ni kuhakikisha tunasaidia vyombo vya ulinzi kwa kutoa taarifa zozote zile ambazo zinaleta tishio la amani ili kuvisaidia vyombo vyetu viweze kuchukua tahadhari na hatua stahiki ili kubaini watu wote wanaotishia kutokuwepo kwa amani katika nchi yetu,” amesema.

Majaliwa amesema lakini pia vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea na wajibu wao wa kuhakikisha kila taarifa inayopatikana lazima ifanyiwe uchunguzi na kubaini wale wote wanaohusika na kama wanapatikana wachukuliwe hatua mara moja.

Amemshukuru Spika kwa maelezo yake ya awali ili kuondoa upotoshaji ambao unaweza kuwa unaendelea na kufanya vyombo vyao vishindwe kufanya kazi yake na kuwavunja moyo watu wanaofanya kazi saa 24 kwa ajili ya ulinzi ambao unawafanya wabaki salama.

MaRC na DC tena bungeni

Katika swali jingine, Mbunge Viti Maalumu, Stella Fiyao amesema nchi inaamini katika uongozi wa kisheria na utawala bora ili kujengwa umoja mshikamano na upendo baina ya wananchi na viongozi wao.

Amesema hata hivyo kumekuwa na changamoto kubwa baina ya baadhi ya wateule wa Rais, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kwa kutumia nguvu na mamlaka yao vibaya kukamata viongozi na wananchi na kisha kuwatupa ndani.

“Moja jambo hili limetengeneza chuki kubwa baina ya wananchi na Serikali yao lakini linafifisha jitihada kubwa za mheshimiwa Rais za kuhubiri 4R na mwisho wa siku jambo hili linakuwa halileti mantiki,” amesema.

Ametaka kujua kauli ya Serikali ni ipi katika kukemea jambo hilo ambalo linatengeneza chuki kubwa baina ya Watanzania na Serikali yao.

“Kauli ya Serikali ni ipi kwa hawa viongozi wanaotumia mamlaka yao kutesa na kunyanyasa wananchi,” amehoji.

Akijibu swali hilo, Majaliwa amesema swali hilo ni linafanana na alilolisema jana Jumatano Mbunge wa Mlimba (CCM), Godwin Kunambi ambapo Dk Tulia aliwapa kazi Serikali kulifanyia kazi.
Рекомендации по теме
Комментарии
Автор

Ipo siku Mungu wetu atashusha kiburi hicho

mtakwaelius
Автор

Mbona huyo spiker anahalalisha watu kufa kwa kutekwa na kuona sawa tu, , hivi dini iko moyoni kwako kweli sio sawa please 😊

alfanikingwan
Автор

Huyu mwanamke tulia ni janga la taifa lazima watanzania tuwe waangalifu na matendo yake ya kubomoa

jamesrobare
Автор

Wasiwasi wangu hapa Kuna kijambo miongoni mwa wanaotuongoza kwa kweli, majibu ya Spika simuelewi.

lusakaone
Автор

Yatakugarimu mbeya kwa uchaguzi .sote ni wazazi mungu atajibu tuombe

fredrickbaryagati
Автор

Spika kakasirika kisa kuuliza tena kwa msisitizo kuhusu watu kupotea😂😂

barnaba
Автор

Spika anasema watu wasiwe na mihemuko kwenye maisha ya watu

pauljulius
Автор

Yaani hata mganga wa kienyeji ana haki ya kuua au kuteka watu bila kuulizwa na serikali??? Ohh Tanganyika yangu.... Una kila kitu lakini uongozi wetu unatufanya tuishi kwa mashaka makubwa. Mungu unatuona watanganyika usituache na uzao wetu tukaangamia. Kumbuka kazi za mikono yako EE Mungu usiyefichwa na chochote. Unayaona yote yaliyo mioyoni mws viongozi uliowaruhusu waongoze kwa kipindi chote hiki.

ariibahati
Автор

Huyu spika jamani ni tatizo.
Inakuwaje mbobezi wa sheria kama anavyojinadi hawezi kutafsiri swali lililo "generalized" na lisilo?
Pia aseme anaodai wanatumia "mihemuko" ni mihemuko inayotokana na uwepo wa jambo lipi na kwa manufaa ya kina nani maana melezo yake spika yanaashiria anajua chanzo cha hiyo mihemuko ya wabunge!
Usalama na haki za watu ikiwemo kuishi ni mambo very serious, hatupaswi kuyashughulikia kwa uzembe, milengo ya kulinda vyeo, vyama vyetu au maslahi mengine binafsi!
Ni aibu spika kunyamazisha mjadala au maswali ya aina hii huku ripoti, tena za vyombo vya dola zikisema mtu au vikundi vya watu wanagundulika kupoteza, kuua na/au kuzika watu wengine pasipo wao walio walinzi wetu kujua. Tujiulize, kama watu hadi 10 wameuwa Singida na mtu au kikundi kimoja, je intelijensia ya vyombo vyetu vya usalama inayosemwa kuwa ya hali ya juu inatumika wakati gani, kwa matukio yapi na kwa manufaa ya nani!!?
Unaangamia Tanzania, nakulilia Tanzania...! 😢

dennisbarongo
Автор

Mbona mbunge kasema wazi, Haja generalize Mambo

tumlakimwaitumule
Автор

Mimi ni ccm lakin kuna kiasira kinapanda kufuani mwangu,
Mpak nawish ningekuwa jetriii

kefamwakipesile
Автор

Huyu spika ni nyoko sana ila mwisho wa siku naye atakufa tu

SauliBasso
Автор

Anaonge kamaatakavyo kwa sababu familia yake ipo salama.

psttitonakazaelimjema.
Автор

Mh Spika ni vema ukatenganisha Bunge na Serikali....Ukweli Bunge lina kazi kubwa kwenye kuisimamia serikali yetu...

godfreylyimo
Автор

Spika uko vizuri. Mimi najuuliza hao walinzi wa amani walikuwa wapi watu wote wakafukiwa na mganga huko Singida.?? Hebu vumua hilo Jeshi la Polisi.Wewe kiongozi mzuri wa kurekebisha mambo

marthaswai
Автор

...Wazirii Kabalansii Maneno Lakini sipika wew Kwasabab Huna kichaa Nyumban kwak Unaonaa Sawaa Tu achaa yakutokee

tonotvonline
Автор

Kiukweli watanzania wa chini tuna changamoto kubwa sana
Sijui kwamba tunajitambua vizur

mbwanarajab
Автор

Ilauzuri wote tunakufa ispokuwa nimda natarehe

KenedyMboma-zbcq
Автор

Waziri mkuu ni mtu mwenye ekima na Adabu kwa watz ni kiongozi asiye kuwa na miemuko ya vyeo wala ana makandokando lakini kuna dada juu ya muimili ni shida walikueoo na wakaondoka na mungu akubaliki waziri mkuu tunajua mfumo umekubana sana ila wewe ni kiongozi safi

eflnmxs
Автор

Huyu Spika ni shida. Swali la kisekta au siyo la kisekta siyo ishu hapo. Waziri Mkuu ndiye kiongozi wa serikali bungeni. Ana wajibu kutoa maelezo.

robertzingu