#TAZAMA| RAIS WA YANGA ENG. HERSI, AHESABIWA

preview_player
Показать описание
Leo, Agosti 26 ikiwa ni siku ya nne tangu kuanza kwa zoezi la Sensa rasmi, Rais wa Klabu ya Yanga, Mhandisi Hersi ametimiza wajibu wake wa kuhesabiwa kama mwananchi.

Mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la kuhesabiwa, Rais wa Yanga amesema zoezi linaendelea vizuri, ingawaje yeye hakupata bahati ya kuhesabiwa siku ya kwanza ya tarehe 23 Agosti, lakini alijiandaa kikamilifu kushiriki na kuwapa ushirikiano wa kutosha makarani wa Sensa.

Hata hivyo, Eng. Hersi, amewataka wananchi kuacha taarifa sahihi majumbani kwa ambao hawajahesabiwa kwani zoezi la sensa linatarajiwa kukamilika ndani ya siku sita au saba, hivyo wale ambao bado hawajahesabiwa watapata fursa hiyo adhimu na muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu.

Follow us on:
FACEBOOK;

INSTAGRAM;

TWITTER;
Рекомендации по теме