RAIS SAMIA AFUNGUKA 'BAADHI YENU MNASHTUMIWA KWA KUTOFANYA HAKI/KESI ZA KUBAMBIKIZWA/UPELELEZI'

preview_player
Показать описание
Ni Agosti 25, 2021 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amehudhuria ufunguzi wa kikao cha Maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi na makamanda wa Polisi wa mikoa/vikosi Dar es Salaam.

“Wafungwa walikuwa 16,542 lakini Mahabusu ni 15,194 mpaka Juzi, sasa Mahabusu hawa kuna walikaa wiki, miaka mitatu, mwaka, muda mbalimbali na kila anaeguswa upelelezi haujakamilika sasa nitoe wito mara mbili”-Rais Samia

“Kwa zile kesi ambazo mna hakika upelelezi hautokamilika hao watu watolewe, wakafaidi huru wao wakiwa nje kama kesi haina mwelekeo basi hao watu watolewe lakini zile kesi ambazo mna uhakika upelelezi utatimia basi ziharakishwe”- Rais Samia

“Kwa upande mwingine Mwanadamu ni Mwanadamu na ana uhuru wake naomba mkae na wadau wengine muangalie uwezekano wa kurekebisha sheria ya kumuweka mtu mahabusu”- Rais Samia

“Tuko hapa kuhudumia watu na si kudidimiza watu, ni aibu kuona kwenye simu zetu tunarushiwa clip Askari wa Jeshi la Polisi anakubaliana na Raia achukue rushwa”- Rais Samia
Рекомендации по теме
Комментарии
Автор

Hilo la kukamata ndio upelelezi ufanyike halijakaa sawa. Uko sawa kabisa Rais wangu kuwa upelelezi kwanza ndo mtu akamatwe na Hilo linawezekana Tena sana tuu. Tunatesa na kuharibu mfumo mzima wa maisha ya watu wasio na hatia kwa kisimgizio cha upelelezi haujakmilika! Tupeleleze

ayubumbembati
Автор

Nimekupenda sana leo mama umeongea vzr

shabanmwambe
Автор

Zuia chanjo haraka isitumike Tanzania haraka

nuhumhagama
Автор

Apo umefanya kweli ao awatupendi wenzao

samsonmwakyembe
Автор

Mheshimiwa Rais tunashukuru kwa kuyaona hayo. Hiyo idadi ya mahabusu nikubwa mno inasikitisha sana, inaokena kuna vitengo havitimizi majukumu yake kabisa

cityonahillstudio
Автор

Waajiriwa wengi ni ukoo ukoo mwingi police wanaajiriana wao kwa wao police wengi anajiunga kufanya kazi police Hajui sheria waliomtangulia nao Hawaijui sheria watu wapo kwa Ajili ya Rushwa yaani

joshuasamson
Автор

Apo nimekuelewa kidogo vpi mboe nae sikabambikiziwa

nyembeseven
Автор

Mama anatumia lugha laini sana, kila kitu mama anaomba, angekuwa anawataka wafanye hayo na yale. Yeye ni amiri jeshi mkuu! Sheria ya mahabusu ingetakiwa ibadilishwe. Watu wawe uraiani isipokuwa kwa makosa ya madawa ya kulevya, uhujumu uchumi, mauaji. Mengine haya sio ishu.

allymapinda
Автор

Hapo ndio utajuwa Nini maana ya administration of justice for all 🤣🤣🤣🤣

husseinkatumpula
Автор

Mheshimiwa rais anawaomba! Hao watu siyo wakuomba kutekeleza maagizo.Wamezoea lugha ya amri.Rais alimuomba Gavana wa benki kuu kupunguza riba hadi leo hatujasikia kama riba imepungua.

serafineslaa