BEMBEA YA MAISHA FULL PLAY (SEHEMU YA KWANZA, ONYESHO I, II & III)

preview_player
Показать описание
MTIRIRIKO WA MAONYESHO
SEHEMU YA KWANZA
Onyesho I

Nyumbani kwa Sara, Sara ameketi kwenye kochi baada ya kumeza vidonge vya
dawa kwa sababu ya maradhi yanayomsumbua. Yona anayeonekana mchovu na
mwenye kukinai anaingia kwa nyumba.
Onyesho linaanza kwa kuonyeshwa namna Yona asivyofurahia hali katika
nyumba yake. Analalamikia Sara kuwa hajamwandalia chakula. Yona
hababaishwi na hali ya Sara ya ugonjwa, haja yake ni chumba kivuke moshi. Sara
anamweleza namna mwili wake ulivyo, hapo mazungumzo kuhusu mwana wao,
Neema, yanaanza. Yona anatoa wazo lake kwa Sara amwite bintiye aje ampeleke
hospitalini. Sara anakataa wazo hilo kwa kukiri kuwa bintiye ana familia yake
ambayo anafaa kuishughulikia.
Maoni ya Sara yanazua mgogoro baina yake na Yona kuhusiana na mtoto wao
Neema. Yona anashikilia kuwa ni jukumu la bintiye kuwajibikia matibabu ya
mamake, naye Sara anashikilia kuwa bintiye ana majukumu ya kwake na tayari
amewafanyia mengi, kwa hivyo, awachwe apumzike.
Mgogoro huu unasawazishwa onyesho linapoelekea kuisha. Sara na Yona
wanakubaliana kuwa wanafaa kumpa binti yao baraka zao.
Onyesho linamalizika kwa kuonyeshwa Yona akirejelea suala la chakula. Sara
anamweleza asubiri kwa kuwa amempelekea Dina salamu aje awafanyie
chochote.

Onyesho II
Onyesho hili linatukia nyumbani kwa Dina. Kiwa alikuwa amefika nyumbani
kumjulia hali mama yake.
Onyesho hili linaanza kwa kuonyeshwa namna Kiwa anavyogusagusa chakula na
kudai ametosheka. Katika harakati ya mazungumzo juu ya chakula, Dina na Siwa
wanajikuta wakizungumza kuhusu familia ya Yona na Sara. Dina anamweleza
mwanawe Kiwa namna familia hiyo ilivyodunishwa na wanajamii kwa kukaa
muda mrefu bila kujaliwa na watoto na hata baada ya kufanikiwa na watoto
wasichana, jamii iliendelea kuwasuta na kuwakejeli kwa kuwa hawakujaliwa na
mtoto wa kiume atakayerithi fimbo ya baba yake. Kusemwa huku na wanajamii
kunasababisha Yona kuingia katika ulevi, ulevi ambao unamsukuma kumdharau
na kumchapa bibi yake kichapo cha mbwa.
Onyesho linaisha kwa kuonyeshwa Dina akimuaga Kiwa ili aweze kwenda
kumsaidia Sara katika harakati ya mapishi kwa kuwa Sara alikuwa anaugua.

Onyesho III
Onyesho hili linatokea nyumbani kwa Sara, jikoni. Dina yupo katika harakati ya
mapishi naye Sara amejikunyata kwenye kibao. Mchuzi u tayari. Sara
anamshukuru Dina kwa kufika kumsaidia. Dina anapokea shukrani na kumpa
Sara maneno ya kumtia nguvu. Dina anamweleza Sara kuwa kila kitu hufanyika kwa mpango wa Manani. Anamweleza atazame faraja ilivyovuka kwake kwa vile
watoto wake wamefaulu maishani. Anampa matumaini kwamba atapona kwa
kuwa hospitali ambayo Neema anampeleka ina watalaamu.
Mazungumzo ya matumaini yanaendelea kunoga huku Dina akiendelea na
mapishi. Dina anauliza Sara alikokwenda Yona na hapo mazungumzo kuhusu
mwanamume na utamaduni yanazuka.
Tunaelezwa namna utamadumi ulivyowajenga wanaume kama watu wasiofaa
kuingia jikoni.
Onyesho hili linatimia Sara akimweleza Dina kuhusu mipango iliyopangwa na
Neema kuhusu namna atakavyorudi kliniki kupata matibabu.

@Papafilipoultimatetv @KatuniZaMorowa
#bembeayamaisha #kiswahilirahisi #tamthilia #animation #cartoon #fullplay fullplay
Рекомендации по теме
Комментарии
Автор

This really helped me understand the set book😊😊 thanks❤

sarahekode
Автор

Aki thanks sana God bless you sasa nitapata A in Jesus name 👩‍🎓

LUYALIMUDIMBA
Автор

Just nice Na Zina mafunzo kuniokolea Nayo wadau kcse nimepata A-kiswahili

MaryannNjoki-gmdm
Автор

Si sara na yona wako kijijini😅😅mbona unaonyesha mandhari ya jijini😢

Hooyoow
Автор

Iko fyn 🙃 I love it slow but understandble❤

harrietsyombua
Автор

Imenisahidia xana Kwa sababu nmeshindwa kusoma vitabu

Benjamin-mr
Автор

aky asante imenifanya nielewe mengi 😊😊😊

josephngetich
Автор

Asante sana kwa sababu nimesoma lakini sijanyita vizuri

FaithNzivo-iypg
Автор

Thank u for helping us now we're same where

josephmbio
Автор

Kazi safi but kama itakuwa possible tufanyie sehemu zingine

agreementtv
welcome to shbcf.ru