MELI ILIVYOPINDUKA ZIWA VICTORIA ASUBUHI YA LEO...

preview_player
Показать описание
Juhudi za kuitoa meli ya Serikali Mv Clarias ndani ya Ziwa Victoria iliyokuwa imepinduka katika bandari ya Mwanza kaskazini zinaendelea ikihusisha timu ya wataalamu mbalimbali wa meli huku chanzo cha kupinduka kwa meli hiyo kikiwa bado hakijafahamika mara moja.

Meli hiyo ya Mv Clarias inayofanya safari zake kutoka katika mwalo wa kirumba jijini Mwanza kuelekea kisiwa cha Goziba Wilayani Muleba Mkoani Kagera imepinduka Ziwa Victoria katika bandari ya Mwanza kaskazini ikiwa haina abiria mapema asubihi ilipokua imeegeshwa eneo hilo .

Chanzo cha kupinduka kwa meli hiyo bado hakijawekwa bayana na mamlaka husika,Afisa uhusiano wa Kampuni ya huduma za meli nchini Abdulrahman Salum amethiitisha kupinduka kwa meli hiyo na jitihada zinazoendelea kwa sasa.
Рекомендации по теме