AJALI DAR: BASI la BURUDANI LAGONGANA na DALADALA MBEZI, MAJERUHI WAKIMBIZWA HOSPITALI....

preview_player
Показать описание
AJALI DAR: BASI la BURUDANI LAGONGANA na DALADALA MBEZI, MAJERUHI WAKIMBIZWA HOSPITALI....

Basi la Kampuni ya Burudani lilikuwa likitokea Tanga kwenda Dar es Salaam limeacha njia na kuparamia vyombo vingine vya usafiri ikiwamo magari matatu, pikipiki tatu na bajaji tatu.
Ajali hiyo imetokea leo Aprili 8, 2023 katika eneo la Kibamba Luguruni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mashuhuda, basi hilo linadaiwa kuwa lilikuwa kwenye mwendokasi hivyo wakati likijaribu kulikwepa gari dogo lililokuwa linaingia barabarani, likapoteza mwelekeo na kuhamia upande wa pili wa barabara na kugonga daladala na bodaboda.

Bado hakujatolewa taarifa za aliyepoteza maisha kwani majeruhi wamewahishwa katika Hospitali ya Poshi iliyopo jirani na eneo hilo.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:

⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 713 750910), ( +255 783453136)

⚫️ OUR PLAYLISTS:
Рекомендации по теме
Комментарии
Автор

Pole sana, Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi majeruhi wapone kwa haraka😭😭

pascha_mwendesha_
Автор

Daaah...!!! Bus la jamaa zangu hili 😭
Huyo mwenye gari dogo alizingua sana yan

otiocyw
Автор

Polen sana majeruh ishallaah
mpone hraka

aminatanzanya
Автор

Poleni sana wasafiri wote mngu awatie nguvu.

CarbonChriphord-pvwf
Автор

Burdan tosha za babu yangu burdan express za mzee wangu

Srt_ally
Автор

Vyeti vya udereva vikaguliwe kwa madaraja yote, sio sahihi kuwaacha madereva wa magari madogo, bajaji na pikipiki maana ajali azichagui madaraja ya leseni. Tuache siasa

erickzephania
Автор

Mungu atawajalia watapona..watajejea..makwao

kagoyemwambal
Автор

Kinga ya kwanza ya ajali ni dereva kudhibiti mwendo wako.

erickchitumbi
Автор

Tatizo sio mwendo kasi tatizo ni hilo gari dogo hata basi la mwendo kasi pia lilisababishwa na hao wa gari ndogo

gabrielkabato