RAIS MAGUFULI ATUA KWA MARA YA KWANZA AIRPORT MPYA CHATO

preview_player
Показать описание
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amewapongeza wananchi wa Chato mkoani Geita kwa kuitikia wito wa Serikali wa kuongeza juhudi katika kazi za uzalishaji mali hata kuiwezesha Wilaya hiyo kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.
Mhe. Raisi Magufuli ametoa pongezi hizo leo Julai mosi, 2019 wakati akiwasalimia wananchi hao katika eneo la Njianda, muda mfupi baada ya kutua uwanja wa ndege wa chato akitokea Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Raisi Magufuli ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa, kushikamana na kutobaguana ili kwa pamoja waijenge tanzania ambayo ina rasilimamli nyingi.

kabla ya kuwasalimu wananchi wa Njiapanda Mhe. Raisi amewasalimu na kuwashukuru wananchi wanaofanaya kazi za ujenzi katika uwanja wa ndege chato.
Mhe Raisi Magufuli amewasili leo katika Kijiji cha Mlimani Wilayani Chato kwa mapumziko.
Рекомендации по теме