filmov
tv
Sirro Asisitiza Denti wa UDSM Aliyeuawa na Polisi ni Jambazi!

Показать описание
Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro, amesema mwanafunzi wa UCC iliyochini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi, alikuwa ni jambazi.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetolea ufafanuzi malalamiko yaliyotolewa na ndugu za kijana huyo aliyeuliwa na jeshi hilo wiki moja iliyopita akidaiwa kujaribu kumpora askari silaha.
Kamishna Simon Sirro amewataka ndugu wa marehemu huyo wakatembelee eneo la tukio kusikia wananchi wanasema nini kuhusiana na kitendo cha kijana huyo ambaye aliuawa na polisi baada ya wenzake kukimbia kusiko julikana.
Amesema katika eneo la tukio palikuwa gari la kubebea fedha lililokuwa likisambaza fedha katika mashine za ATM za CRDB kiasi cha Tsh. 320, 000,00 ambapo mtuhumiwa huyo kwa kushirikiana na wenzake alidaiwa kutaka kufanya tukio la uvamizi katika gari hilo, kabla ya askari kumuwahi na kumuua.
Tangu kutokea kwa tukio hilo, ndugu wa marehemu huyo wamegoma kuchukua mwili wake kwa ajili ya maziko wakidai kuwa ndugu yao ambaye pia alikuwa ni mwanafunzi wa UDSM hakuwa muhalifu, huku wakitaka jeshi hilo liombe radhi kwa kudai kuwa ndugu yao alikuwa mhalifu.
Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya…

Комментарии