filmov
tv
Maandamano ya Renamo mjini Maputo yazuiliwa kwa mabomu ya machozi
Показать описание
Siku moja baada ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Msumbiji, chama cha upinzani cha Renamo kimefanya maandamano Ijumaa katika mji mkuu Maputo, kupinga matokeo hayo. Maandamano hayo yalizuiliwa kwa mabomu ya kutoa machozi yaliyotupwa na Kikosi cha Haraka cha Kudhibiti Ghasia cha polisi huko Jamhuri ya Msumbiji, wakati waandamanaji wakitaka kuelekea katika Baraza la Katiba kupinga matokeo hayo kwa amani. Msumbiji ilifanya uchaguzi wa serikali za mitaa Oktoba 11.
Vyama vikuu Frelimo, Renamo na Democratic Movement for Change (MDM) vilichuana katika manispaa 65.
Siku ya Alhamisi, Oktoba 26, matokeo ya mwisho yalitangazwa, yakiwapa ushindi mkubwa Frelimo lakini wenye kupingwa katika manispaa 64.
#mozambiqueelections #renamo #frelimo #mozambique #maputo