Shabiki Yanga Awazodoa Simba kipigo cha Jwaneng 'watafungwa sana'

preview_player
Показать описание
Shabiki Yanga Awazodoa Simba kipigo cha Jwaneng 'watafungwa sana'

SIMBA imeondoshwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu huu baada ya kuruhusu kufungwa bao 3-1 nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Hiyo ni baada ya kuruhusukufungwa mabao matatu nyumbani na kufanya uwiano wa mabo kuwa 3-3 baada ya kushinda 2-0 ugenini hivyo wameondolewa kwa kanuni ya bao la ugenini.

Kipindi cha kwanza cha mechi hiyo, Simba ilionekana kulishambulia mara kwa mara lango la Jwaneng lakini Ubora wa kipa wao Ezekiel Morake uliifanya Simba kuondoka ba bao moja pekee lililofungwa na Rally Bwalya dakika ya 40.

Bao hilo la Bwalya lilitokana na John Bocco kupiga pasi kwa Bernard Morrison katikati ya Uwanja aliyekimbia na mpira mbele na kupiga pasi mpenyezo kwa Bwallya akapiga chenga mabeki wawili wa Jwaneng na kuingia kwenye boksi kisha kupiga shuti la wastani lililozama nyavuni.

Morrison, Shomari Kapombe, Hassan Dilunga, Bocco, Sadio Kanoute na Bwalya ni miongoni mwa wachezaji wa Simba walioweza kutengeneza nafasi za mabao na kupiga langoni kwa Jwaneng kipindi cha kwanza katika nyakati tofauti lakini kipa Ezekiel akaokoa mashuti yao.

Mphoyamodimo Keiponye na Thabo Leinanyane wote wa Jwaneng ndio wachezaji waliooneshwa kadi za njano katika dakika 45 za kwanza huku kukiwa hakuna kadi nyekundu kwa pande zote mbili.

Рекомендации по теме
Комментарии
Автор

Kwani Rivers ansijuwa Nani Ile ya Nigeria

kassidpandu
Автор

Wameshindwa hata kupigana hata kwa kijiko Bora wangefia ughaibuni tukakwaakodia ndege ya kuwarudisha lakini wamefia uani kwao ni kuwanyanyua na kuwaingiza ndani hakuna gharama kubwa. Hao ndiyo makoloooo

burilomalima