filmov
tv
'HOUSE GIRL' ALIYE MWAGIWA MAFUTA YA TAA NA BOSS WAKE, MAPYA YAIBUKA, MARAFIKI WAFUNGUKA MAZITO
Показать описание
Dunia ina mambo mengi, mengine yanaweza kukuacha mdomo wazi kwa kushangaa, kusikitika na pengine kuumiza. Hii ni simulizi ya mfanyakazi wa ndani aliyemwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto ni miongoni mwa mambo ya kuumiza.
Ungana nami katika kisa hiki cha kusikitisha.
Ikiwa zimepita siku mbili tangu kuripotiwa taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kumshikiria mfanyabiashara na mkazi wa Usagara wilayani Misungwi mkoani humo, Christina Shiriri (43) kwa tuhuma za kumfanyia ukatili mfanyakazi wake wa ndani Grace Joseph (17) kwa kummwagia mafuta ya taa mwilini kisha kumchoma moto akimtuhumu kumwibia fedha kiasi cha Sh161,000.
Tukio hilo limetokea Juni 4, 2024 katika Kata na Tarafa ya Usagara Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza ambapo Christina alidai kuibiwa fedha zake alizokuwa amehifadhi chumbani kwake ambapo baada ya kumuuliza binti huyo anadai alikiri kuchukua fedha hizo ambapo hata hivyo alimrejeshea ndipo mwajiri huyo kuanza kumfanyia ukatili huo kwa kumchoma moto mikono yote, tumbo pamoja na mapaja yake yote.
Binti huyo mpaka sasa anaendelea kuuguza majeraha na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi huku mtuhumiwa akiendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Ndugu, jamaa na majirani wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesimulia namna tukio hilo ilivyotokea.
Mwanyekiti wa Kitongoji cha Isera Kijiji cha Indetemiha Kata ya Usagara mkoani Mwanza, Elikana Masanja amesema kwa mujibu wa taarifa za majirani binti huyo alikuwa na siku tatu aanze kazi.
Hata hivyo amesema baada ya tukio hilo kutokea hakupewa taarifa hiyo hadi alipokuja kusikia kutoka kwa raia wema na kuchukua wamuzi wa kwenda eneo la tukio ambapo hata hivyo aliishia kubisha geti ambalo halikufunguliwa.

Комментарии