filmov
tv
WASHIRIKI WA KOZI YA UONGOZI KUTOKA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI WALIDHISHWA NA MAENDELEO YA MTWARA
Показать описание
Washiriki wa kozi ya uongozi kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi kilichopo Dar Es salaam, wamepongeza hali ya maendeleo ya mkoa wa Mtwara huku wakikili kuwa hali hiyo imechagizwa na Sera nzuri zilizowekwa na Serikali.
Akizungumza na Faida Online tv baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Boma uliopo kwenye Ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mtwara kilichowahusisha viongozi mbalimbali ndani ya mkoa huo leo Januari 13 2024, Breg. Gen. Erick Muhoro ambae ni Mkufunzi mwelekezi Mwandamizi mambo ya anga kutoka chuo hicho cha Ulinzi, amesema kuna mambo yaliyosababisha wauchague Mkoa huo wa Mtwara.
Breg. Muhoro ametaja mambo hayo kuwa ni pamoja na Mafanikio yaliyopatikana kupitia zao la Korosho, Uwepo wa Gesi asilia hali inayosaidia kwenye mambo ya Nishati safi, na watatwmbelea Msimbati kuona Visima vya Gesi.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mtwara Col. Patrick Kwnan Sawala, amesema Pato la Mkoa wa Mtwara kwa mwaka 2023 limepanda na kufikia Shilingi Trilioni 5.2 kutoka Shilingi Trilioni 4.7 kwa mwaka 2022 hii ni kwa mujibu wa takwimu za BOT.
Hata hivyo RC Sawala ameongeza kuwa Pato la Wananchi limepanda kutoka Milioni 2.7 mwaka 2022 mpaka kufikia Milioni 3.04 kwa mwaka 2023.
Washiriki hao watakuwepo Mtwara kwa kipindi cha wiki moja.