filmov
tv
ZITTO Akitoka Mahakamani Leo/ Baada ya Dhamana
Показать описание
ZITTO Akitoka Mahakamani Leo
MBUNGE wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu -Dar leo Novemba 2, akitokea Kituo cha Polisi Mburahati ili kusomewa mashtaka yanayomkabili baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi na kukaa rumande tangu Oktoba 31, 2018.
Zitto anatuhumiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu mauaji ya baadhi ya askari polisi na wananchi katika kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza mkoa wa Kigoma ambapo baada ya kukamatwa alipelekwa kwenye Kituo cha polisi cha Oysterbay, kabla ya kuhamishiwa polisi kati na baadaye kulazwa kwenye kituo cha polisi Mburahati.
Kabla ya kukamatwa na Polisi, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno, alimtaka Zitto kuwasilisha alichokiita, “vielelezo vya madai yake,” kuwa watu zaidi ya 100 wameuwa katika eneo la Uvinza