filmov
tv
USAJILI WATIKISA DIRISHA DOGO BONGO, BWALYA, YONDANI, BALEKE NDANI
Показать описание
Usajili wa dirisha dogo Tanzania Bara umefunguliwa Disemba 15, mwaka huu na tayari tumeshuhudia baadhi ya timu zikitambulisha wachezaji wao wapya waliowanasa kwenye dirisha hilo huku wengine wakianza kuzitumikia timu zao kwenye mechi za Ligi Kuu.
Mwananchi Digital imekuletea mkusanyiko wa usajili wa dirisha dogo ambazo zimeshakamilika mpaka sasa na baadhi ya tetesi ambazo ziko mbioni kukamilika.
Kama inavyofahamika Simba tayari imemsajili mkongomani, Elie Mpanzu wakati Yanga wakimalizana na nyota wa zamani wa Simba, Israel Patrick Mwenda akitokea Singida Black Stars.
Winga wa zamani wa US Gendemarie na RS Berkane ya Morocco, Victorien Adebayo ametua Singida Black Stars, huku kiungo wa zamani wa Tabora United, Najim Mussa akijiunga na Namungo FC kwa mkopo kutoka Singida Black Stars.
Naye, beki wa zamani wa Azam FC, Daniel Amoah amejiunga na Namungo FC huku KenGold ikiwanasa wachezaji wanne ambao ni Sadala Lipangile kutoka Biashara United, Abdallah Nassir wa Miembeni ya Zanzibar, Mathias Juviliani kutoka KVZ ya Zanzibar na Sambale Komanje wa Tabora United.
Klabu ya Pamba ya Mwanza haijakaa kinyonge katika dirisha hili kwani tayari imekamilisha usajili wa wachezaji wanne akiwemo mshambuliaji wa Singida Black Stars, Habib Kyombo na winga, Deus Kaseke ambao walicheza mchezo uliopita dhidi ya KMC. Mwingine ni beki wa kushoto, Sharif Ibrahim kutoka Cameroon na winga wa zamani wa Coasta Union na Singida Black Stars, Hamad Majimengi.
Mabosi wa Pamba hawatanii na wamedhamiria kubaki Ligi Kuu, kwani wanajiandaa kuwaanika nyota wao wanne wa kigeni ambao ni kipa wa Sierra Leone, Mohammed Camara aliyekuwa Singida Black Stars, mshambuliaji Mkenya, Mathew Teggisi Momanyi, Viungo Rally Bwalya kutoka Zambia na Mrundi Tshassiri Nahimana, wamo wazawa winga wa Tanzania Prisons, Zabona Mayombya na beki kisiki, Kelvin Yondani.
Tetesi nyingine katika usajili wa dirisha dogo ni mshambuliaji wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi, Saido Ntibazonkiza anayehusishwa kujiunga na wachimba dhahabu wa Mbeya, Ken Gold ambao wanapambana kujinasua na hatari ya kushuka draja.
Wengine ni kiungo Kelvin Nashon anayetakiwa na Yanga, huku mshambuliaji wa Yanga mkongomani Jean Baleke anayetajwa huenda akatemwa dirisha hili anahusishwa kwenda Namungo kuungana na kocha wake wa zamani, Juma Mgunda.
Tetesi nyingine zinazoendelea kutikisa mpaka sasa ni aliyekuwa kocha wa Yanga, Muargentina Miguel Gamondi anayehusishwa na Singida Black Stars kwenda kuchukua mikoba iliyoachwa wazi na Patrick Aussems aliyetupia virago huku Yanga wakiwa kwenye mazungumzo na kipa wa Pamba Jiji, Yona Amosi.
Naye, kinda wa Simba, Salehe Karabaka aliyekosa nafasi kwenye kikosi cha Fadlu Davids yuko kwenye mipango ya kusajiliwa na KMC, wakati Fountain Gate FC ikiwa kwenye hatua za mwisho za kuwasajili beki wa Tabora United, Said Mbatty na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Coastal Union na Biashara United, Yusuph Athuman.
Kwa leo ni hayo tu kutoka kwenye usajili na tetesi za usajili wa dirisha dogo la Ligi Kuu Bara, endelea kufuatilia Mwananchi Digital kuhusiana na usajili katika dirisha hilo.
Mimi ni Damian Masyenene wa Mwananchi Digital

Комментарии