Binadamu aliyevunja rekodi kwa urefu (maajabu ya dunia)

preview_player
Показать описание
Leo katika historia tunakuletea maajabu ya binadamu mrefu zaidi kuwahi kutokea duniani kwa mujibu wa kitabu cha record za dunia cha guiness
Mtu huyu alikuwa anatambulika kama Robert Pershing Wadlow au kwa jina la utani
‘’The Alton Giant’’
Robert alizaliwa February 22 mwaka 1918 Alton Illinois nchini Marekani
Robert alizaliwa na tatizo ambalo kitaalamu linatambulika kama Hyperplasia tatizo lililofanya homoni zake zinazochochea ukuaji kuongezeka kwa kasi ya ajabu na kuwa nyingi kuliko kawaida jambo lililofanya akue kwa kasi ya ajabu kuliko mtoto wa kawaida

Akiwa na miaka nane tu Robert tayari alikuwa na urefu usiopungua futa sita na uzito wa takribani kilo 77 hii ni pamoja na kuwa na uwezo wa kumbeba mtu mzima
Akiwa na miaka 13 tu Robert tayari alikuwa na urefu usiopungua wa futi 7 na inch 4 na kuvunja rekodi na kuwa mvulana wa skauti mrefu zaidi rekodi ambayo anaishikilia mpaka leo hii
Robert alivunja rekodi ya dunia na kuwa mtu mrefu Zaidi duniani baada ya kufikia urefu usiopungua futi 8 na inchi 11 ambayo ni sawa na sentimita 272 au mita 2.72 kwa maana hiyo Robert alibakiza sentimita 33 tu kufikia usawa wa urefu wa goli la mpira wa kikapu lenye urefu wa futi 10 au sentimeta 305
Ingelazimu pia mtu mrefu kama Hasheem Thabeet kusimama juu ya kiti kirefu ili kuweza kufikia urefu wa Robert

Urefu haukumuacha salama Robert kwani pamoja na kuvunja rekodi za dunia na kumpa sifa kedekede changamoto kadhaa zilimuandama Robert mfano kwenye gari la familia ilibidi atengewe siti ya peke yake upande wa nyuma na siti ya mbele yake ilibidi iondolewe ili aweze kunyoosha miguu yake vizuri

Robert pia alivunja rekodi ya kuwa na mguu mkubwa kuwahi kutokea duniani na alikuwa anavaa kiatu size namba 75 ilibidi kampuni moja ya viatu ya Marekani kujitolea kumtengenezea Robert viatu vyake maalum

Changamoto nyingine iiliyomuandama Robert ilikuwa ini kushindwa kutembea vizuri kwani alilazimika kutumia fimbo maalum ili kumsaidia kusimama na kutembea vizuri.

Kutokana na ukubwa wa umbo lake Robert pia alikosa dawati na kiti akiwa shule na ikalazimu uongozi wa shule kumtengenezea dawati lake maalum ili kukidhi mahitaji ya ukubwa wa umbo lake.

Background Music:
Elf Meditation Preview by Kevin MacLeod

#maajabu #thestorybook #bongobiz
Рекомендации по теме
welcome to shbcf.ru