#TAZAMA| WALICHOKIFANYA POLISI KUKOMESHA UHARIFU DAR

preview_player
Показать описание
Jeshi la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na technolojia limepanga kuja na mkakati wa Pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam katika maswala ya tafiti mbalimbali ambazo zimelenga kubaini na kukomesha vitendo vya kiharifu.

Akiongea na waandishi wa Habari mkuu wa chuo cha taaluma ya Polisi Dar es salaam, SACP. Lazaro Mambosasa amesema moja ya majukumu yao ni kulinda rai ana mali zao ambapo amebainisha kuwa kupitia kitengo cha utafiti katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam wameona vyema wafike chuoni hapo ili kujifunza maswala ya kiutafiti.

Aidha Mambosasa amewambia waandishi kuwa malengo ya Mkuu wa Jeshi hilo IGP. Camillus Wambura ni kuona Jeshi la Polisi linawekeza katika tafiti ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo limepanga kuingia makubaliano na chuo cha taaluma ya Polisi Dar es salaam Pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam.

Follow us on:
FACEBOOK;

INSTAGRAM;

TWITTER;
Рекомендации по теме