Wazaramo vanga - mama (Mama Huyo)

preview_player
Показать описание
Wazaramo ni kabila la watu kutoka eneo la Dar es Salaam, baina ya Rufiji na Bagamoyo, nchini Tanzania. Mwaka 2000 idadi ya Wazaramo ilikadiriwa kuwa 656,730 [1]. Lugha yao ni Kizaramo. Katika eneo la Rufiji wanajulikana pia kwa jina la Wamyagatwa.

#wazaramomama #vangamamahuyo #wazaramovanga
Wazaramo ni sehemu ya Wabantu. Mababu wanaaminika waliingia katika eneo la Tanzania katika milenia ya kwanza BK. Historia yao ya kimdomo inasema ya kwamba walihamia pwani katika mazingira ya Dar es Salaam kutoka Uluguru (Morogoro) katika karne ya 18.

Walipokaa kwenye pwani walikuwa karibu na makazi ya Waswahili wakaanza kufahamiana na Waislamu. Taarifa za wakoloni Wajerumani mwanzoni mwa karne ya 20 zinaonyesha ya kwamba wakati ule Uislamu ulikuwa umeenea kati ya Wazaramo na waliendelea kujiunga nayo haraka [2]. Siku hizi idadi kubwa wa Wazaramo ni Waislamu.

Jiji la Dar es Salaam lilikua haraka na kumeza vijiji vingi vya Wazaramo na wengine walihamia jijini wakitafuta kazi.
Рекомендации по теме