UCHAMBUZI: Kukamatwa kwa Mbowe na Viongozi 5 wa Chadema

preview_player
Показать описание
UCHAMBUZI: Kukamatwa kwa Mbowe na Viongozi 5 wa Chadema

UCHAMBUZI: Ukichambua kuhusiana na kitendo cha Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na viongozi wenzake watano wa chama hicho kupelekwa katika mahabusu ya Segerea baada ya kunyimwa dhamana katika kesi yao waliyosomewa Machi 27, Katika Mahakama ya Kisutu Dar.

Mbowe na wenzake walifikishwa Mahakamani na kusomewa mashtaka manane ikiwemo kufanya maandamano yaliyosababisha kifo cha Mwanafunzi wa Chuo cha NIT, Akwilina Akwiline, Feb 16 mwaka huu, uasi na kuhamasisha chuki.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, washtakiwa wote walikana ambapo Wakili Nchimbi alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.

Pia, Nchimbi aliwasilisha maombi kwa mahakama hiyo ili washtakiwa wasipewe dhamana kwa sababu ya usalama wa umma wa Watanzania ambapo washtakiwa walipelekwa Segerea na kesi yao itaendelea tena Machi 29, mwaka huu.

Рекомендации по теме
Комментарии
Автор

Huwezi amini haya yote lengo ni moja tu!

fnk
Автор

nitailinda na kuitetea katiba hicho ndio kiapo cha viongozi wetu

sadamomary
Автор

Mtakanyingi naswaba humkuta mwingi msibaa

shekhahamed
Автор

kbx mzee baba maana hawana adabu mdomoni.

dadileonard