filmov
tv
Moreno Batamba -Mapenzi ya Shida

Показать описание
Ajiko Toyambi alias Moreno Batamba alizaliwa 1955 huko Kisangani, DRC akifariki 1993 akiwa na umri wa miaka 38....
Baada ya kuacha Shule Mwaka 1971, Alijiunga Katika Bendi Ya Orchestra Maquis Sasa Bata kabla ya kuhamia Uganda 1974, akijiunga Katika Bendi Ya Orchestra Bana Ngenge, Iliyokuwa Ikiongozwa Na Mwimbaji Jojo Ikomo ambamo walirekodi nyimbo nyingi tajika.
Bana Ngenge Au Kwa Jina Jingine Ilikuwa Ikitwa Bana Moja, Katika Miaka Ya 1970 Iliondoka Kampala Wakaenda Katika Jiji La Nairobi Nchini Kenya.
Baadhi Ya Wanamuziki Waloiunda Bendi Hiyo Ilikuwa Ni Pamoja Na Watunzi Na Waimbaji Jojo Ikomo, N'dala Mobangi, Beya Maduma, Roxy Tshimpaka, Fataki Lokassa Losi Losi ‘Masumbuko Ya Duniya’, Makwanzi Duki, Kuka Mwana Bitala Na Hassan Omari miongoni mwa wengine.
Mwaka 1972 Bendi Hiyo ilivunjika huku Wanamuziki Wengi Wakiondoka.
Mwanamuziki Fataki Lokassa Alisafiri Akiwa Na Bendi Ya Bana Ngenge Wakaingia Tanzania Ambako Kwa Bahati Mbaya Mwaka 1975, Wanamuziki Wa Bendi Hiyo Wakagawanyika.
Mgawanyiko Huo Uliifanya Bendi Hiyo Kufa Na Kuwafanya Wanamuziki Moreno Batamba Na Jojo Ikomo Wakaenda Kujiunga Katika Bendi Ya Les Noirs Mwaka 1976.
Moreno Batamba Aliwahi Kuishi Katika Jiji La Dar Es Salaam Kati Ya Miaka Ya 1978 Hadi 1980, Akitunga Na Kuimba Katika Bendi Ya Orchestra Safari Sound (Oss), Kabla Ya Kurudi Tena Nairobi.
Mwaka Wa 1980 Moreno Alianzisha Bendi Ya Orchestra Moja One, Akiwa Safu Ya Wanamuziki Akina Coco Zigo Mike, Mpiga Gitaa Siama Matuzungidi, Mcharanga Drum Lava Machine Na Wengine Wengi Waliotoka Katika Bendi Ya Shika Shika.
Nyimbo Hizo Zilikuwa Za "Pili Mswahili", "Dunia Ni Duara”, " "Mapenzi Ya Shinda", "Mwanamke Hatosheki", Urembo Si Hoja” Na "Angela " Zilizorekodiwa Mwaka 1981 Na "Urembo Si Hoja.
Kibao Cha "Pili Muswahili" Kilikuwa Mahsusi Kwa Ajili Ya Rafiki Yake Wa Kike Aliyejulikana Kwa Majina Ya Pili Mikendo Kassim.
Pili Alikuwa Mtanzania Waliyekutana Naye Alipokuwa Katika Bendi Ya Orchestra Les Noirs Katika Mji Wa Mombasa Mwaka 1976.
Moreno Kwa Kipindi Kifupi Alijiunga Katika Bendi Ya Orchestra Virunga Ya Samba Mapangala Mwaka 1983.
Bendi Ya Orchestra Virunga, Yaelezwa Kuwa Ilikuwa Ni Bendi ‘Nyota’ Iliyoweza Kupiga Muziki ‘Live’ Katika Baadhi Ya Kumbi Za Jiji Hilo.
Iliwashirikisha Wanamuziki Wengine Wakiwemo Akina Coco Zigo, Fataki Lokassa, Dago Mayombe Na Baadae Moreno Batamba, Ottis Na Samba Mapangala.
Moreno Batamba Alikuwa Akipendelea Zaidi Kutunga Na Kuimba Nyimbo Zake Kwa Lugha Ya Kiswahili. Nyimbo Zake Zilikuwa Zikigusa Hisia Za Jamii Zote.
Aidha Aliimba Wimbo Wenye Mahadhi Ya Taarabu Baada Ya Kuimba Wimbo Wa “Vidonge Sitaki” Akiwa Katika Kikundi Ch Golden Star Mwaka 1993.
Kwa Mapenzi Ya Mungu Nguli Huyo Moreno Batamba Alifariki Mwaka Huo huo 1993, Akiwa Na Umri Mdogo Wa Miaka 38.
Mapenzi ya shida ni wimbo katika albamu Vidonge sitaki (1993) ..
Bonyeza SUBSCRIBE kupata video zaidi....

Комментарии