SEKESEKE LA UCHAGUZI 2025 LANUKIA LISSU AMWANDIKIA BARUA MNYIKA, MBOWE NAYE...

preview_player
Показать описание
Joto la uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limeanza kufukuta, huku likiibuka swali la nani kati ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu atapitishwa kuipeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi hiyo.

Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, ameshaonyesha kusudio la kuwania wadhifa huo na tayari ameshamwandikia barua Katibu Mkuu, John Mnyika kuonyesha nia yake.

Sio siri tena, nia yake hiyo ameiweka wazi hata katika mahojiano mbalimbali aliyoyafanya katika vyombo vya habari, akisema amemwandikia Mnyika barua ya nia ya kugombea urais 2025 na nia ya kuwania nafasi aliyonayo sasa ndani ya chama hicho.

Mnyika amelithibitishia Mwananchi kwamba tayari barua ya Lissu imemfikia na itafuata taratibu za chama. Katika barua ya Lissu, ameonesha nia pia ya kutetea nafasi yake ya umakamu mwenyekiti kwenye uchaguzi ujao.

Wakati mambo yakiwa hadharani kwa upande wa Lissu, taarifa ambazo Mwananchi linazo kutoka ndani ya chama hicho, Mbowe ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chadema, anatajwa kuwania tena urais mwakani.

Licha ya kukaa kimya na hata alipoulizwa na Mwananchi mara kadhaa hakujibu lakini duru za siasa zinaeleza naye ni miongoni mwa wanaoweza kukata tiketi ya kuomba ridhaa ya Chadema kuwania kiti cha urais.

Mwananchi linazo taarifa za ndani kuwa Mbowe atajitosa kuwania nafasi hiyo na tayari Lissu mara kadhaa amekuwa akisema ikitokea nafasi anayokusudia kuiwania, Mbowe ataitaka basi atamwachia.

“Kaka hilo la urais halina ubishi mpaka sasa ni Mbowe na umakamu bara ataendelea Lissu, hata kama kutakuwa na mtu hataki hatutakubali sijui Lissu asigombee urais, asigombee umakamu, hilo halipo,” alisema mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, huku  akiomba asitajwe jina. Aliongeza:

“Ukiwaweka kwenye mizania na siasa za sasa za Rais Samia (Suluhu Hassan) Mbowe ni mtu sahihi, Lissu sawa ila si wakati huu. Lissu atarudi jimboni akasaidie bungeni wakati Mbowe akiwa anakwenda Ikulu.”

Chanzo hicho kilidokeza zaidi kwa kusema: “Hatutakuwa na mgombea mwingine zaidi ya hawa, Mbowe au Lissu. Hatutakuwa na mgombea sijui ametoka CCM au wapi. Mwaka huu tumejipanga wenyewe na kama itatokea Mbowe akasema hataki, Lissu ataendelea lakini Mbowe akijitosa tu imekwisha.”

Mjumbe mwingine wa kamati alisema: Jambo  linalowatofautisha wawili hao ni rasilimali fedha. Mwamba (Mbowe) ana fedha bwana, haitakuwa jambo gumu. Fikiria operesheni za kurusha chopa na magari anatoa fedha zake mwenyewe.”

Halitakuwa jambo jipya kwa yeyote kati yao kuwania urais, kwa nyakati tofauti walishawahi kushiriki kinyang’anyiro hicho, Mbowe katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na Lissu aligombea mwaka 2015.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Mbowe alipata kura 668,756 akishika nafasi ya tatu dhidi ya kura 9,123,952 za mshindi wa kiti hicho aliyekuwa mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete. Nafasi ya pili ilishikwa na Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyepata kura 1,327,125.

Wakati wa Lissu nao mambo yalikuwa hivyo hivyo, aliukosa urais kwa kupata kura 1,933,271 akishika nafasi ya pili dhidi ya mgombea wa CCM, John Magufuli aliyetetea wadhifa huo kwa kura 12,516,252 sawa na asilimia 84.

Hata hivyo, wagombea wote hawana historia ya kushiriki au kufanya siasa nje ya Chadema, wote walisikika wakiwa upinzani na umaarufu wao wa kisiasa umetokana na chama hicho.

Katika historia ya Chadema, haikuwahi kurudia kumsimamisha mgombea aliyeshiriki kinyang’anyiro hicho, jambo linaloibua swali Je, mwakani kitamrejesha aliyewahi kushindwa nafasi hiyo?
Комментарии
Автор

KELELE NYINGI KUMBE KUNA MOTO KWA WAPOTOSHAJI 😢😢😢😢😢

OmmyJames-xnji