Unamkumbuka Joseph Kaniki ‘Golota’..? alitamba na Simba, akiifunga Yanga

preview_player
Показать описание
Ni ‘Mwamba’ aliyewahi kutamba na Simba SC mwanzoni mwa miaka ya 2000 akisifika kwa mashuti na kuwa na bahati ya kufunga kwenye mechi ya watani wa jadi #DerbyYaKariakoo.

Mwaka 2001 ndio nyakati ambazo Kaniki alizitikiza nyavu za Yanga mara mbili. Alianza Septemba 1, 2001 kwenye mechi ya Ligi Kuu ambapo Simba ilishinda goli 1-0. Kisha Septemba 30, 2001 kwenye michuano ya Muungano, Kaniki alifunga tena katika matokeo ya 1-1.

Nyota huyo yupo mjini na sasa anawafua vijana wake wa Mshikamano Talent Academy

#Kaniki #Golota