HUYU NDIYE Layla Khalfan Atokwette ALIYESHIKA NAFASI YA PILI WASICHANA KIDATO CHA NNE 2021

preview_player
Показать описание
Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya pili kwa wasichana katika Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2020 Nchini Tanzania Layl Khalfan Atokwete mwenye umri wa miaka 17 aliyesoma katika shule ya Canossa iliyupo Jijini Dar-es-Salaam ametoa wito kwa Serikali juu ya uboreshwajia wa miundombinu na wanafunzi kujituma zaidi.

Tumefanya mahujiano na Mama wa Binti Layl khalfan Atokwete anasema ni mtoto wake wa pili kuzaliwa Kati ya watoto wa tatu alikuwa na juhudi na mdadisi toka akiwa mtoto mdogo. Namshukuru Mungu kwa hatua hii.

Matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), yameonyesha ongezeko la ufaulu kwa wahitimu waliopata daraja la kwanza kwa alama saba.
Daraja hilo maana yake ni mtahiniwa kufaulu masomo saba kwa alama A. Daraja la kwanza lina alama saba hadi 17, huku daraja la pili likiwa na alama 18 hadi 21 na daraja la tatu likiwa na alama 22.
Комментарии
Автор

Hongera sana Layla mwanangu, . Hongera rafiki zangu Reynalda na Khalfan kwa matokeo mazuri ya mtoto. Mungu wetu atukuzwe daima.

dr.mastidia