RAIS SAMIA KUSHIRIKI MKUTANO WA FOCAC UTAKAO FANYIKA JIJINI BEIJING CHINA

preview_player
Показать описание
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (Forum on China-Africa Cooperation-FOCAC) utakaofanyika jijini Beijing, China kuanzia tarehe 4 hadi 6 Septemba 2024. Dkt. Samia Suluhu Hassan anashiriki mkutano huu kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping.
Mkutano huu wa 9 wa FOCAC utafungulia na Raia Xi Jinping ambapo, hotuba yake ya ufunguzi itatoa uelekeo wa China katika uhusiano wake na nchi za Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nchi zaidi ya 40 kati ya 54 za Bara la Afrika watashiriki Mkutano huo. Viongozi wengine mashuhuri watakaoshiriki mkutano huo ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonia Guterres; Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mhe. Moussa Faki na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi A. Adesina.

Katika mkutano huo, Serikali ya China imemteua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhutubia kwenye hafla ya ufunguzi akiiwakilisha Kanda ya Afrika Mashariki.

Mkutano huo wenye kaulimbiu “Kushirikiana ili Kuendeleza Usasa na Kujenga Jamii Bora ya China na Afrika kwa Mustakabali wa Pamoja” (Joining Hands to Advance Modernization and Build a High-Level China-Africa Community with a Shared Future utagawanyika kwenye Mikutano Minne ya Ngazi ya Juu ambayo itafanyika kwa muda mmoja. Kila Mkutano utajadili mada moja ambazo ni Utawala wa Nchi (State Governance); Mpango wa Miundombinu na Uwekezaji (Belt and Road Initiative); Maendeleo ya Viwanda na Kilimo cha Kisasa (Industrialization and Agricultural Modernization); na Amani na Usalama (Peace and Security).

Tanzania itajikita kwenye mada ya Maendeleo ya Viwanda na Kilimo cha Kisasa. Mada hii imezingatia Mpango wa Maendeleo wa Tatu wa Miaka Mitano (Third Five Year Development Plan) ambao ndiyo mpango wa mwisho wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya 2025.

#michuzihabari

#MichuziTV #KaziIendelee

KWA HABARI MBALIMBALI TEMBELEA:

JE, UNA HABARI?

Рекомендации по теме