ACHENI MBWEMBWE FANYENI KAZI, TUPELEKE WAGOMBEA WAZURI' HAPI AFUNGUKA AKUMBUSHA VIONGOZI WASIJISAHAU

preview_player
Показать описание
Katibu Mkuu wa Umoja wa wazazi Jumuiya ya chama cha mapindizi CCM Taifa Ally Hapi (MNEC) amewataka viongozi wa jumuiya ya wazazi na viongozi wa chama hicho kuhamasisha wananchi wenye sifa ya kuwa viongozi bora wagombee nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa ili wasaidie katika kupeleka mbele maendeleo ya wananchi kwenye maeneo yao

Hapi alisema hayo wakati akizungumza na wananchi na wanachama wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Pwani baada ya kuwasili kwa ziara ya siku nne inayolenga kuimarisha jumuiya ya wazazi na kuimarisha chama cha Mapinduzi CCM ambapo alisema jumuiya za chama ni sehemu katika kuhakikisha chama kinashuka kwa wananchi waendelee kukiamini na kukipa ushindi kwenye chaguzi zote zijazo na kukifanya kiendelee kushika dola.

"Ndugu zangu nawapongeza sana kwa mapokezi makubwa mliyotupa katika mkoa huu wa pwani mmetuonesha mahaba makubwa ambayo hayana mfano,sisi tumekuja kwa ziara ya siku nne yenye lengo la kujenga Jumuiya ya wazazi na kuimarisha chama cha mapinduzi pamoja na kueleza kazi zilizofanywa na serikali ya CCM chini na uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan"alisema Hapi

Alisema ili chama cha mapinduzi kiweze kushinda ni lazima kuwa na wagombea wanaokubalika na wananchi ili wakitangazwa kusiwe na nongwa na kuwafanya wanachama kuwapa kura wagombea wa vyama vingine kutokana na hasira hivyo ni muhimu kwa kuandaa watubwanaokubalika.

Mbali na kuwa na watu sahihi wa kugombea Hapi alisema ni wajibu wa jumuiya zote zinawajibu wa kuhakikisha wanaongeza wananchama na huku akisema jumuiya ya wazazi imekuwa na kiongozi kwa jumuiya zingine katika Usajili wa wanachama kielekroniki kwa kusajili wanachama milioni 2.2 ikifuatiwa na jumuiya ya wanawake ambao wamesajili wanachama 1.5 na jumuiya ya vijana ikisajili wanachama 1.2 jambo ambali ni muhimu katika ukuaji wa chama.

"Malengo ya chama chetu ni kuhakikisha tunaendelea kushinda katika chaguzi zote kuanzia uchaguzi wa aerikali za mitaa na uchaguzi Mkuu wa mwakani 2025,hivyo ndugu viongozi tunaowajibu wa kuhakikisha tunaongeza wanachama kwa kuwasajili kielektroniki ili kuwa na wananchama watakaokipa ushindi chama katika chaguzi"alisema Hapi

Aidha Hapi aliwapongeza wanachama kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kukijenga chama cha mapinduzi pamoja na mshikamano ulipo kati ya chama na serikali ambao ndiyo msingi wa kutashinda uchaguzi kutokana na umoja uliopo miongoni mwa wanachama.

"Msisitizo na maelekezo ya mwenyekiti wetu wa chama anatuka sote kwa pamoja kutanguliza maslahi ya chama mbele kwa usemi huu 'chama kwanza mtu baadae' ikiwa na maana kuwa katika kila jambo masilahi ya chama ni lazima yawe mbele kwa kushikamana pamoja na kujitafakari ikiwa mambo yanayofanyika yanakijenga chama"alisema
Kuhusu utatuzi wa kero za wananchi Katibu Mkuu Hapi aliwataka viongozi wa chama na jumuiya kushuka chini kwenda kwa wananchi kutatua kero za wananchi zao kwani huo ndiyo wajibu wa chama cha mapinduzi.

"Twende kwa wananchi tukasikilize kero zao bila mbwembwe zinazoweza kuwafanya wananchi wasituelewe lakini mbwembwe zetu ziwe katika kueleza mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita na kutatua matatizo yao tofauti na watu wengine,tusipofanya hivyo watu watakichukia cha na kuwapa kura watu wengine"alisema Hapi
Комментарии
Автор

CCM ni chama changu nakiombea kitawale Tanzania milele.

omarybakunda
Автор

Anajua kuwa tayari wanayo matokeo FEKI ya kila kituo

faustinluambano
visit shbcf.ru